Monday, 16 March 2015

KUPENDEZA NA KUWA STYLISH NI ZAIDI YA KUVAA

Ni vi zuri watu kupendeza na kwenda na wakati na ili mtu upendeze lazima uzingatie vitu vingi na muhimu hapa tunaangalia rangi ya nguo, make up, viatu, nywele, mapambo, umbo au shep ya mvaaji na vingine vingi.
 Jambo kubwa la kuzingatia au kuwaza kabla ya kufanya hayo yote lazima ujue unaenda wapi, kuna shughuli gani, na wakina nani watakuwepo  eneo ilo pia wewe mvaaji unanafasi gani au wewe ni nani kwenye jamii.
 Watu  wengi wamekuwa wakivaa mavazi tofauti tofauti maeneo mbalimbali na kuonekana hawaendi na wakati kwani wanakuwa hawavai kutokana na mazingira au tukio husika lakini wao wenyewe wanajiona wako sahihi na wamependeza.
  Kama nlivyosema apo awli kupendeza na kuwa stylish ni zaidi ya kuvaa, kujiremba na mambo mengine mengi.

  Kujiamini pia kunamfanya mtu aonekane stylish na aliyependeza hata kama atakuwa amevaa  kawaida sana, watu wengi wana poteza kujiamini wanapo kuwa wamevaa nguo walizozichagua wao na kujikuta wao tofauti kna watu wengine kwenye eneo husika, jaribu kujiamini na present your self, hata kama wewe ndo ulotokelezea tofauti kutokana na utakavyo onyesha kujiamini ndivyo utakavyo pia kwa watu wengine.


No comments:

Post a Comment